Monday, December 19, 2016
Sunday, December 18, 2016
BREAKING NEWS!!
Diwani wa Chadema Kata ya Boma Jimbo la Mafinga Mjini ndugu Kisoma amesimamishwa Udiwani na Tume ya Uchaguzi ya Taifa baada ya kuthibitika hajui kusoma na kuandika.
Friday, December 16, 2016
SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA SEKTA YA KILIMO INATOA MCHANGO KATIKA KUFIKIA NCHI YENYE UCHUMI WA VIWANDA
Na.Immaculate Makilika.
SERIKALI kupitia Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi imesema kuwa imeandaa mikakati mbalimbali ili
kuhakikisha Sekta ya Kilimo inatoa mchango zaidi katika kufikia nchi ya
uchumi wa kati.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam
jana katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoandaliwa na kituo cha televisheni cha TBC, aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ambaye sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya
Ulinzi Dkt. Florence Turuka alisema kuwa Serikali imeandaa mikakati hiyo
ili kuhakikisha kunakuwepo na uzalishaji wa mazao ya kilimo ili viwanda
viweze kupata malighafi, chakula cha kutosha pamoja na ajira kwa
wananchi.
“Serikali imeamua kuanzisha
viwanda vidogo vya kuchakata mazao kwa ajili ya soko, kushirikisha sekta
binafsi katika kuongeza thamani ya mazao, ili kuvutia wakekezaji katika
sekta ya kilimo nchini” alisema Dkt. Turuka.
Kwa mujibu wa Dkt. Turuka alisema
ili kuhakikisha huduma za ugani zinakua za kisasa Serikali
inadhamiria kutumia simu za mkononi zitakazorahisisha utoaji wa taarifa
kwa wataalamu wa kilimo, ikiwa ni pamoja na kusaidia wakulima kupata
huduma za kitaalamu kwa wakati.
Aidha Dkt. Turuka alisema
mikakati mingine inayotekelezwa na Serikali ni pamoja na kuongeza idadi
ya matrekta hadi kufikia 6,000 badala ya 400 yaliyokuwepo awali.
Aliongeza kuwa Serikali
imekusudia pia kujenga maghala karibu na maeneo yanayozalisha mazao ya
matunda na mbogamboga ili kuweza kuyahifadhi kwa muda kabla mazao hayo
hayajapekelekwa sokoni ili kupunguza uharibifu.
Naye Katibu Mkuu wa sasa wa
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mathew Mtigumwe alisema
Serikali itaboresha mfumo wa takwimu wa wataalamu wa kilimo pamoja na
kuwajengea uwezo ili kusaidia utekelezaji wa maendeleo ya kilimo katika
maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Serikali inawakaribisha
wawekezaji wa kilimo cha miwa ambapo imeandaa zaidi ya hekta 6000 kwa
ajili ya kilimo hicho nchini.
WATAYARISHAJI FILAMU WATAKIWA KUWA WABUNIFU.
Na. Genofeva Matemu.
Watayarishaji wa kazi za ubunifu ikiwemo filamu Tanzania wamehaswa kuwa wabunifu na kuacha kunakili kazi ambazo zilishafanywa na watu wengine kwani kwa kufanya hivyo hupelekea kudidimiza sekta ya Filamu na kuidhalilisha tasnia ya uigizaji nchini.
Watayarishaji wa kazi za ubunifu ikiwemo filamu Tanzania wamehaswa kuwa wabunifu na kuacha kunakili kazi ambazo zilishafanywa na watu wengine kwani kwa kufanya hivyo hupelekea kudidimiza sekta ya Filamu na kuidhalilisha tasnia ya uigizaji nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Ado Mapunda alipokua akifunga
warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu na michezo ya
kuigiza iliyofanyika kwa siku tatu na kufungwa leo Mkoani Mara.
“Tumieni
fursa hii ya kipekee kuchota maarifa ya kutosha yatakayowaongezea ujuzi katika
kazi zenu za filamu. Naamini baada ya warsha hii mtalenga kutoa kazi bora
zitakazokidhi mahitaji ya wadau wenu na pia zitakazoweza kushindana kwenye soko
la ndani na kimataifa” amesema Bw. Mapunda
Kwa upande wake Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao ameiomba
Ofisi ya Mkoa wa Mara na Wilaya zake kushirikiana na kuhimiza Sekta ya
Utamaduni kutengewa fedha kwa ajili ya maendeleo ya Filamu huku wakijumuishwa
katika fursa mbalimbali ikiwepo mikopo kupitia mfuko wa vijana na wanawake
ambapo itasaidia vijana na wanawake wengi
ambao wanajishughulisha na Tasnia ya filamu Kwa kuwa filamu inaweza kuchangia
ustawi wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja na pia kuchangia pato la nchi kwa kiwango
kikubwa.
Naye katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce
Fisoo amewaomba watayarishaji wa kazi za filamu kuwasilisha miswada yao kabla
ya kuandaa filamu zao ili bodi ya filamu ipate fursa ya kupitia miswada hiyo na
kuiboresha kabla ya filamu kuandaliwa jambo ambalo litasaidia kuondokana na
filamu zitakazokua zinazuiliwa kutokana na makosa madogo madogo yanayojitokeza
katika filamu zao.
Aidha
watayarishaji wa Mkoa wa Mara wametakiwa kutumia maarifa ya warsha hiyo
kutengeneza filamu zinazohamasisha uwajibikaji, umuhimu wa elimu kwa mtoto wa
kike, athari za ukeketaji, athari za uvuvi haramu kama baadhi ya maeneo ambayo
jamii ya Mkoa wa Mara inahitaji kuelimisha na kuondokana na dhana potofu.
Mafunzo
hayo yameshirikisha zaidi ya wadau wa sekta ya filamu na michezo ya kuigiza 200
kutoka Mkoa wa Mara, Halmashauri ya Manispaa ya Mosoma, Musoma Vijijini, Bunda
Mji, Tarime Mji, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Lorya, Butihama na wadau
kutoka Mkoa jirani wa Simiyu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Rashid Taka
na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Raphael Siumbo kufanya uchunguzi na
kuwachukulia hatua watendaji wote watakaobainika kuhusika katika uuzwaji wa
kiwanja cha shule ya msingi Waso.
Ametoa
agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Desemba 15, 2016) wakati akihutubia wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Waso Wilaya ya Ngorongoro
akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha.
Waziri
Mkuu alisema Serikali haiwezi kuvumilia kuona watendaji wachache wasiokuwa
waadilifu wanamega kiwanja cha shule na
kukiuza kwa maslahi yao, hivyo aliwataka viongozi hao kufuatilia na kumpa
taarifa ya hatua za kisheria walizochukua kwa wahusika.
“Mkuu
wa wilaya na Mkurugenzi hapa kuna malalamiko ya viwanja fuatilieni viwanja
hivyo vinavyolalamikiwa na wananchi ni viwanja gani je hiyo ya kwamba mmeuza
viwanja vya shule ameuziwa nani,” alisema.
Aidha,
Waziri Mkuu amemtaka Bw. Taka ahakikishe Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na
Mzingira, Bw. Switbeth Byorushengo anatekeleza majukumu yake ipasavyo. Ametoa
agizo hilo baada ya wananchi kudai Ofisa huyo ameshindwa kufanya kazi na
kumuomba Waziri Mkuu aondoke naye.
Alisema
Bw. Byorushengo anatakiwa kuhakikisha halmashauri hiyo inapima viwanja vya
kutosha na kutoa hati kwa wananchi ili waweze kupata maeneo ya kujenga makazi
na shughuli zingine za kijamii.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw.
Byorushengo kuhakikisha halmashauri hiyo inaanza ujenzi wa hospitali ya wilaya
na ifikapo Aprili, 2017 awe amepewa taarifa za ulipofikia ujenzi huo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi huyo alisema tayari wapo katika mchakato wa ujenzi wa
hospitali ya wilaya ambapo wametenga sh. milioni 800 za kuanzia.
Akizungumzia
kuhusu mgogoro wa ardhi kati ya vijiji vya Tarafa ya Loliondo na Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti, Waziri Mkuu alitoa muda wa siku 30 kwa uongozi wa Shirika
la Hifadhi za Taifa Nchini (TANAPA) wawe wamekamilisha uhakiki wa mpaka huo.
Naye
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambaye ni Mbunge wa Ngorongoro
Mheshimiwa William Ole Nasha alimuomba Waziri Mkuu kuwasaidia kutatua mgogoro
huo wa ardhi kwa kuwa ni wa muda mrefu na unakwamisha shughuli za maendeleo.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo alisema Wilaya ya Ngorongoro
inachangamoto nyingi ikiwemo ya ardhi na sasa kuna mgogoro kati ya Kampuni ya
Thomson Safari na wananchi ambao wanadai kuwa ardhi hiyo ilichukuliwa kinyemela
na mwekezaji huyo bila ya wao kushirikishwa.
Alisema
baada ya ziara ya Waziri Mkuu kumalizika mkoani hapa atarudi wilayani
Ngorongoro kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali ikiwemo ya ardhi na matumizi
mabaya ya fedha zinazotolewa na wawekezaji ambazo matumizi yake hayajulikani.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, DESEMBA 16, 2016.
MWILI WA BRIGEDIA JENERALI MHAIKI WAAGWA RASMI LEO.
JPM APONGEZWE URATIBU MAAFA KAGERA.
Na. Joseph Martin,
Nottingham
WATANZANIA bado
tuko katika masikitiko kufuatia maafa yaliyoletwa na tetemeko la ardhi mkoani
Kagera na baadhi ya maeneo ya Kanda ya Ziwa. Tetemeko hilo tunaambiwa ni la
kiwango cha skeli ya 5.7 ambayo ni kubwa.
Watu 17
wamefariki kutokana na tetemeko hilo, mamia wamejeruhiwa na maelfu ya nyumba
ama zimebomoka au zimeharibika kwa namna tofauti. Mimi binafsi nina ndugu zangu
ambao ni waathirika wa tukio hili na namshukuru Mungu kwa misaa waliyopata.
Nimefuatilia
sana yanayotokea kule Kagera na naendelea kufuatilia kwa sababu jamaa zetu wa
kule kwa kweli wanahitaji msaada wetu ingawa na wao pia wanapaswa kuchukua
hatua zao na za jamaa zao wa karibu katika kujinasua na janga lililowafika.
Maoni yangu leo
si ya kueleza tukio hilo wala kufafanua maafa yalivyowagusa ndugu, jamaa na
marafiki zetu, bali kimsingi, nimeandika kufikisha ujumbe kwa Mhe Rais wa Awamu
ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli. Nitaeleza kwa nini Dkt. Magufuli anapaswa
kupewa hongera zake katika hili.
Mosi, tufahamu
kuwa hili ni janga la asili na ni jambo
ambalo wanasayansi wanasema halitabiriki na hakuna mtu anaweza kujua lini
tetemeko la ardhi litatokea. Lakini hata tukijua, bado ni ngumu kuzuia athari
zake hasa kwa makazi na miundombinu.
Lakini tangu
kutokea kwa jambo hili, labda tofauti na ilivyopata kutokea katika majanga
mengine nchini kama vile mafuriko ya Kilosa na majanga mengine ya tetemeko au
mafuriko, kwa mara ya kwanza, na ikiwa haina uzoefu bado wa muda mrefu katika
uongozi, Serikali ya Magufuli imetuunganisha na imetutendea haki sana kwa
kiwango chake.
Mara tu baada ya
tukio, Waziri Mkuu alifika Kagera kuwajulia hali waathirika, kushiriki mazishi
ya umma ya waliofariki na kutoa maagizo kwa watendaji wake juu ya hatua za
haraka za kufanywa.
Mara tu baada ya
Waziri Mkuu kutoka Kagera, Rais Magufuli ambaye hata baadhi ya watendaji wake
waandamizi walishakuwa mjini Lusaka, Zambia alikokuwa aende kwa ajili ya
sherehe za kuapishwa Rais Lungu, naye aliahirisha safari hiyo.
Rais aliahirisha
safari na kubaki Dar es Salaam kuratibu kwa karibu maafa hayo na namna ya
kuwasaidia waathirika. Na mara moja tuliona athari za uwepo wake nchini ambapo
ilifanyika harambee Ikulu ambapo watanzania tukahamasishwa kuchangia.
Serikali ikachukua
hatua muhimu za mawasiliano na hamasa kwa wadau ikiwemo kutangaza akaunti ya
maafa na namba za simu za sisi kuchangia. Akaunti hizi, tofauti na miaka ya
nyuma zimesambazwa sana katika mitandao ya kijamii na hata nimeona matangazo
katika magazeti na katika televisheni. Mkuu wa Mkoa wa Kagera anatoa taarifa za
mara kwa mara pia.
Serikali pia
kupitia taasisi na wizara mbalimbali pia imeendesha matukio mengine ya
kuchangia waathirika, imeratibu nchi nyingine za kigeni na Balozi kupeleka
misaada Kagera na misaasa hiyo imeanza kuwafikia waathirika.
Nafahamu kuwa
Serikali haikuwa na wajibu wa moja kwa moja katika hili kwa kuwa haikusababisha,
lakini juhudi hizi ni za kupongezwa sana na za kukumbukwa sana. Mzee Magufuli
Mungu akutangulie.
Nnitumie fursa
hii pia kuwasihi watanzania wenzangu, katika kuwasaidia wenzetu, kama
tulivyoanza, kusiwe tena na siasa wala watu kutafuta upungufu na kukosoa. Kila
mmoja wetu “ajiongeze” wanasema vijana wa
mjini.
Hata kwa ndugu zangu
waathirika nao pia tujue sisi na jamaa zetu tuna jukumu la kwanza katika hili
na tujitume kujinasua katika janga hilo, Serikali inaweza kuleta kidogo cha
kuchangia au kutufuta machozi, au kurekebisha miundombinu ya umma lakini
tusibaki watu wa kusubiri tukidhani ndio tutafanyiwa kila kitu.
Hakuna
Serikalini duniani inayoweza kufanya kila kitu hasa yanapotokea majanga makubwa
hata ziwe na uwezo vipi. Niliwahi kufika Marekani kwenye eneo la janga la
Septemba 11 pale Manhttan, New York na kukuta hata baada ya miaka 10 eneo lile
halikuwa limeweza kurejea katika hali yake ya awali.
Kuna eneo kule
Japan baada ya maafa ya mafuriko nimepata kuvikuta vikiwa hadi leo haviko
katika sura yake ya awali. Naamini hata ndugu zangu wa Kagera wajue hili, yapo
mambo yanaweza kufanyika yakawa bora zaidi kwa jitihada zao na za Serikali,
lakini pia yapo yanayoweza kuchukua muda zaidi na au hata yasirejee katika
hatua kama za awali.
Nihitimishe, hongera
kwa JPM lakini pia Serikali na wadau wengine tuendeleze moyo huu huu na
ushirikiano huu huu katika matukio mengine mengi zaidi yawe ya maafa au ya
kawaida. Kama tulivyoungana katika suala la madawati na hili la maafa, naamini
tukiendelea kuungana pamoja, Tanzania itasonga mbele.
Nawashukuru
sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)







