Na. Joseph Martin,
Nottingham
WATANZANIA bado
tuko katika masikitiko kufuatia maafa yaliyoletwa na tetemeko la ardhi mkoani
Kagera na baadhi ya maeneo ya Kanda ya Ziwa. Tetemeko hilo tunaambiwa ni la
kiwango cha skeli ya 5.7 ambayo ni kubwa.
Watu 17
wamefariki kutokana na tetemeko hilo, mamia wamejeruhiwa na maelfu ya nyumba
ama zimebomoka au zimeharibika kwa namna tofauti. Mimi binafsi nina ndugu zangu
ambao ni waathirika wa tukio hili na namshukuru Mungu kwa misaa waliyopata.
Nimefuatilia
sana yanayotokea kule Kagera na naendelea kufuatilia kwa sababu jamaa zetu wa
kule kwa kweli wanahitaji msaada wetu ingawa na wao pia wanapaswa kuchukua
hatua zao na za jamaa zao wa karibu katika kujinasua na janga lililowafika.
Maoni yangu leo
si ya kueleza tukio hilo wala kufafanua maafa yalivyowagusa ndugu, jamaa na
marafiki zetu, bali kimsingi, nimeandika kufikisha ujumbe kwa Mhe Rais wa Awamu
ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli. Nitaeleza kwa nini Dkt. Magufuli anapaswa
kupewa hongera zake katika hili.
Mosi, tufahamu
kuwa hili ni janga la asili na ni jambo
ambalo wanasayansi wanasema halitabiriki na hakuna mtu anaweza kujua lini
tetemeko la ardhi litatokea. Lakini hata tukijua, bado ni ngumu kuzuia athari
zake hasa kwa makazi na miundombinu.
Lakini tangu
kutokea kwa jambo hili, labda tofauti na ilivyopata kutokea katika majanga
mengine nchini kama vile mafuriko ya Kilosa na majanga mengine ya tetemeko au
mafuriko, kwa mara ya kwanza, na ikiwa haina uzoefu bado wa muda mrefu katika
uongozi, Serikali ya Magufuli imetuunganisha na imetutendea haki sana kwa
kiwango chake.
Mara tu baada ya
tukio, Waziri Mkuu alifika Kagera kuwajulia hali waathirika, kushiriki mazishi
ya umma ya waliofariki na kutoa maagizo kwa watendaji wake juu ya hatua za
haraka za kufanywa.
Mara tu baada ya
Waziri Mkuu kutoka Kagera, Rais Magufuli ambaye hata baadhi ya watendaji wake
waandamizi walishakuwa mjini Lusaka, Zambia alikokuwa aende kwa ajili ya
sherehe za kuapishwa Rais Lungu, naye aliahirisha safari hiyo.
Rais aliahirisha
safari na kubaki Dar es Salaam kuratibu kwa karibu maafa hayo na namna ya
kuwasaidia waathirika. Na mara moja tuliona athari za uwepo wake nchini ambapo
ilifanyika harambee Ikulu ambapo watanzania tukahamasishwa kuchangia.
Serikali ikachukua
hatua muhimu za mawasiliano na hamasa kwa wadau ikiwemo kutangaza akaunti ya
maafa na namba za simu za sisi kuchangia. Akaunti hizi, tofauti na miaka ya
nyuma zimesambazwa sana katika mitandao ya kijamii na hata nimeona matangazo
katika magazeti na katika televisheni. Mkuu wa Mkoa wa Kagera anatoa taarifa za
mara kwa mara pia.
Serikali pia
kupitia taasisi na wizara mbalimbali pia imeendesha matukio mengine ya
kuchangia waathirika, imeratibu nchi nyingine za kigeni na Balozi kupeleka
misaada Kagera na misaasa hiyo imeanza kuwafikia waathirika.
Nafahamu kuwa
Serikali haikuwa na wajibu wa moja kwa moja katika hili kwa kuwa haikusababisha,
lakini juhudi hizi ni za kupongezwa sana na za kukumbukwa sana. Mzee Magufuli
Mungu akutangulie.
Nnitumie fursa
hii pia kuwasihi watanzania wenzangu, katika kuwasaidia wenzetu, kama
tulivyoanza, kusiwe tena na siasa wala watu kutafuta upungufu na kukosoa. Kila
mmoja wetu “ajiongeze” wanasema vijana wa
mjini.
Hata kwa ndugu zangu
waathirika nao pia tujue sisi na jamaa zetu tuna jukumu la kwanza katika hili
na tujitume kujinasua katika janga hilo, Serikali inaweza kuleta kidogo cha
kuchangia au kutufuta machozi, au kurekebisha miundombinu ya umma lakini
tusibaki watu wa kusubiri tukidhani ndio tutafanyiwa kila kitu.
Hakuna
Serikalini duniani inayoweza kufanya kila kitu hasa yanapotokea majanga makubwa
hata ziwe na uwezo vipi. Niliwahi kufika Marekani kwenye eneo la janga la
Septemba 11 pale Manhttan, New York na kukuta hata baada ya miaka 10 eneo lile
halikuwa limeweza kurejea katika hali yake ya awali.
Kuna eneo kule
Japan baada ya maafa ya mafuriko nimepata kuvikuta vikiwa hadi leo haviko
katika sura yake ya awali. Naamini hata ndugu zangu wa Kagera wajue hili, yapo
mambo yanaweza kufanyika yakawa bora zaidi kwa jitihada zao na za Serikali,
lakini pia yapo yanayoweza kuchukua muda zaidi na au hata yasirejee katika
hatua kama za awali.
Nihitimishe, hongera
kwa JPM lakini pia Serikali na wadau wengine tuendeleze moyo huu huu na
ushirikiano huu huu katika matukio mengine mengi zaidi yawe ya maafa au ya
kawaida. Kama tulivyoungana katika suala la madawati na hili la maafa, naamini
tukiendelea kuungana pamoja, Tanzania itasonga mbele.
Nawashukuru
sana.
No comments:
Post a Comment